Rais wa Comoro ashinda muhula wa nne wa miaka 5 licha ya shutuma za udanganyifu, Azali Assoumani anaibuka mshindi kwa 62.97% ya kura.
Matokeo yaliyotangazwa jana jioni yanaonesha Assoumani ameshinda kwa asilimia 62.7 ya kura. Upinzani mara moja umeyapinga matokeo hayo ukilalamika kwamba uchaguzi wote uligubikwa na dosari ikiwemo vituo kufungwa kabla ya muda uliowekwa kisheria.
Mmoja ya wanagombea watano wa upinzani Mouigni Baraka Soilihi, amesema hawawezi kuyakubali matokeo yaliyotangazwa kwa sababu ya hitilafu zilizoshuhudiwa ikiwemo tuhuma za wizi wa kura. Tume ya uchaguzi imeyapinga madai hayo ya upinzani.
Rais Assoumani amekuwa madarakani tangu mwaka 2016 na alirefusha muhula wake kupitia mabadiliko tata ya katiba ya mwaka 2019, yaliyoondoa sharti la nafasi ya urais kuwa ya kupokezana miongoni mwa visiwa vitatu vikubwa vinavyounda Jamhuri ya Comoro.