Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro ametangaza Jumatatu wiki moja ya maombolezo ya kitaifa baada ya Kimbunga Chido kupiga kwenye kisiwa jirani cha Ufaransa cha Mayotte ambapo mamlaka inahofia vifo vya “mia kadhaa”, haswa katika miji ya mabanda inayokaliwa na watu wengi wa Comoro.
“Maombolezo ya kitaifa ya wiki moja yametangazwa nhi nzima, kuanzia Jumatatu Desemba 16 hadi Jumapili Desemba 22, 2024, kufuatia kimbunga cha Chido kilichosababisha wahanga wengi na uharibifu mkubwa wa mali kwenye visiwa vya Comoro, haswa katika kisiwa cha Ufaransa cha Mayotte. “, kulingana na agizo kutoka kwa Rais Assoumani Azali.
Kisiwa dada cha visiwa hivyo, Mayotte, kilichoharibiwa siku ya Jumamosi na upepo wa zaidi ya kilomita 220 kwa saa, kilichagua kubaki chini ya milki ya Ufaransa kupitia kura mbili za maoni mnamo mwaka 1974 na mwaka 1976 wakati wa kutangazwa kwa uhuru wa Comoro.
Ikitenganishwa na kilomita 70 pekee na kuwa idara ya Ufaransa mnamo mwaka 2011, Mayotte ina idadi rasmi ya watu ambao nusu ni wageni kulingana na takwimu za hivi punde kutoka taasisi ya takwimu ya kitaifa ya Ufaransa, ambapo ilikuwa watu 123,000 mnamo 2017, 95% kati yao walikuwa Wacomoro.
Hii ni bila kuhesabu watu wengi wanaofika kisiwani humo wakitumia vyombo vinavyosafirisha watu kinyume cha sheria viitwazo “kwassa kwassa”, jina la mitumbwi ya Comoro.