Rais wa Iran ameonya kwamba “uvamizi mdogo zaidi” wa Israel utaleta jibu “kubwa na kali”, wakati eneo hilo likijiandaa kulipiza kisasi kwa Israeli baada ya shambulio la Iran mwishoni mwa juma.
Rais Ebrahim Raisi alizungumza katika gwaride la kila mwaka la jeshi ambalo lilihamishwa hadi kambi kaskazini mwa mji mkuu, Tehran, kutoka eneo lake la kawaida kwenye barabara kuu katika viunga vya kusini mwa mji huo.
Mamlaka ya Irani haikutoa maelezo ya kuhamishwa kwake, na TV ya serikali haikuitangaza moja kwa moja, kama ilivyokuwamiaka iliyopita.
Wakati haya yakijiri Rais wa Israel Isaac Herzog amefanya mazungumzo na mawaziri wa mambo ya nje wa Uingereza na Ujerumani mjini Jerusalem, akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufanya kazi kwa “ukaidi” dhidi ya vitisho vya Iran.
“Ulimwengu mzima lazima ufanye kazi kwa uhakika na kwa ukaidi dhidi ya tishio la utawala wa Iran ambao unalenga kudhoofisha uthabiti wa eneo zima,” Herzog alisema katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake.