Rais wa Kongo Felix Tshisekedi amemuondoa mkuu wa majeshi na maafisa wengine wakuu wa jeshi katika moja ya mabadiliko makubwa katika miaka ya hivi karibuni yaliyofanywa na kiongozi huyo.
Amri ya rais iliyosomwa kupitia kituo cha televisheni ya taifa haikueleza sababu ya kuondolewa kwa mkuu huyo ya majeshi Christian Tshiwewe Songesha, na nafasi yake kuchukuliwa na Luteni Jenerali Jules Banza Mwilambwe.
Wataalamu wa masuala ya jeshi na ulinzi wanadhani, kwamba kuteuliwa kwa Luteni Jenerali Banza Mwilambwe Jules, anaetokea kwenye kikosi cha ulinzi wa rais, kama mtangulizi wake, huenda hapatakuwa na mafanikio zaidi kwenye vita vinavyoendelea mashariki mwa nchi hiyo kwa zaidi ya miaka miwili sasa.
“Lazima kuweko na maboresho”
Kuna wale wanaodhani kwamba, mabadiliko stahiki, ni yale yanayoanzia kwenye ngazi za chini na kupanda juu, kama anavyosema Patrick Mundeke, mwanasiasa na pia mchambuzi wa masuala ya ulinzi.
“Ilikutegemea mabadiliko kwenye uwanja wa mapigano, lazima kuweko na maboresho ya hali ya maisha ya wanajeshi, kuweko na uongozi wa jeshi hii ni kulingana na shirika la habari la DW