Rais wa Namibia Hage Geingob alizikwa katika makaburi ya Heroes’ Acre nchini humo Jumapili kufuatia mazishi ya kitaifa yaliyohudhuriwa na viongozi wa Afrika, rais wa Ujerumani na Princess Anne, dadake Mfalme Charles III wa Uingereza.
Geingob alifariki mapema mwezi huu akiwa na umri wa miaka 82 alipokuwa akipokea matibabu ya saratani. Alikuwa rais wa tatu wa Namibia tangu ilipopata uhuru kutoka kwa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini mwaka 1990. Kabla ya hapo, nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ilikuwa koloni la Ujerumani.
Mjane wa Geingob, Monica Geingos, alitoa ujumbe katika ibada ya kumbukumbu siku ya Jumamosi akitoa heshima kwa mumewe aliyeinuka kutoka wanyenyekevu, wa vijijini na kuwa kiongozi wa taifa lake na mtu anayeheshimika sana katika bara la Afrika.
“Ulizaliwa ukiwa mkulima na ukafa kama rais,” Geingos alisema kwenye ibada ya ukumbusho kwenye uwanja wa soka uliokuwa umejaa waombolezaji.
Katika mazishi yake siku ya Jumapili, jeneza la Geingob liliwekwa kwenye bendera ya Namibia na kubebwa katika sanduku la kioo nyuma ya trela ya kijeshi.
Wawakilishi kutoka nchi 27 walihudhuria mazishi hayo, akiwemo Princess Anne, Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, Rais wa Qatar Tamim bin Hamad Al Thani na wakuu 18 wa nchi. Viongozi wa Afrika Kusini, Angola, Botswana, Kenya, Zambia na Zimbabwe wote walihudhuria.