Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema amesikitishwa na vitendo vinavyoripotiwa vya unyanyasaji kwa baadhi ya Raia wa Nigeria na Waafrika wengine wanaojaribu kuikimbia Ukraine ambapo jumla ya Raia 4,000 wa Nigeria bado wamekwama Ukraine.
Kupitia ukurasa wa Twitter, Ofisi ya Rais wa Nigeria imesema Polisi na Maafisa wa Usalama wa Ukraine wameripotiwa kukataa kuwaruhusu Raia wa Nigeria na Nchi nyingine za Afrika kupanda mabasi na treni kuelekea mpaka wa Ukraine na Poland.
“Kundi moja la Wanafunzi wa Nigeria ambao wamekataliwa mara kwa mara kuingia Poland wamehitimisha kuwa hawana namna ila kusafiri tena kupitia Ukraine na kujaribu kuondoka nchini kupitia mpaka na Hungary, watendewe kwa utu na bila upendeleo”
“Wote wanaokimbia hali ya migogoro wana haki sawa ya kupitishwa kwa usalama chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa na rangi ya pasipoti zao au ngozi zao hazipaswi kuleta tofauti”
BREAKING: RAIS PUTIN AIBUA MAPYA, AAMURU VIKOSI VYENYE SILAHA ZA NYUKLIA VIKAE TAYARI
KAMA MOVIE: WANAJESHI WA UKRAINE NA URUSI WAKIPAMBANA KWA SILAHA MITAANI ‘MAJIBIZANO YA RISASI’