Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi, anadaiwa kuhusika na kushindikana kwa miradi mikuu unaohusika na kashfa ya “Tuna,”.
Hayo yameelezwa na mmiliki kampuni ya Emarati na Lebanon ya utengenezaji meli ya Privinvest, katika mahakama kuu ya Uingereza.
Kampuni ya Privinvest, na mmiliki wake kutoka Ufaransa, Iskandar Safa, wanakabiliwa na kesi ya dola bilioni 3.1 kutoka taifa hilo la Afrika kwa shutuma za kulipa mamilioni ya dola za rushwa kwa maafisa wa Msumbiji, na benki za Credit Suisse.
Msumbiji inadai zaidi ya dola milioni 136 zililipwa ili kupata upendeleo wa kufanya miradi mitatu kati ya mwaka 2013 na 2014, ikijumuisha mmoja kutumia vibaya ukanda wa bahari wa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa samaki aina ya jodari.
Tuhuma hizo dhidi ya Rais Nyusi huenda zikatia dosari juhudi zake za kutetea kiti chake cha Urais katika uchaguzi ujao.
Uchaguzi mkuu nchini Msumbiji umepangwa kufanyika tarehe 9 Oktoba mwaka ujao wa 2024.
Serikali ya Maputo imetangaza kuwa, wapiga kura nchini humo wanatarajiwa kupiga kura kumchagua rais wao mpya na wabunge na viongozi wengine katika mikoa tarehe tisa ya mwezi Oktoba mwaka wa 2024.
Chama tawala cha Frelimo kilishinda kwa kura nyingi katika uchaguzi mkuu wa urais wa mwaka wa 2019 baada ya kupata asilimia 73 ya kura zilizopigwa.