Rais wa Ufaransa, anatarajiwa kufanyia bazara lake la mawaziri mabadiliko, kwa kumteua waziri mkuu mpya, wandani wa rais Emmanuel Macron, wakisema analenga kuipa serikali yake sura mpya.
Ni mabadiliko yanayotarajiwa jumatatu hii, ambapo rais Macron analenga kuipa serikali yake muonekano mpya baada ya kukosolewa kwa kipindi kirefu.
Wajibu wa waziri mkuu Elisabeth Borne, umeonekana kukubwa na matatizo tangu muswada wa uhamiaji uliokuwa unashinikizwa na rais Macron kuangushwa bungeni mwaka uliopita, japo baadae ulipitishwa kwa kufanyiwa marekebisho.
Macron ambaye anazidi kupata upinzani mkali kutoka kwa mrengo wa Kulia unaoongozwa na Marine Le Pen, amekutana na Borne usiku wa kuamkia leo, afisi yake ikisema wamejadili swala la mafuriko kaskazini mwa Ufaransa, ila wadidisi wa siasa wanasema huenda pia mabadiliko ya bazara la mawaziri yanayotarajiwa.
Borne ambaye amehudumu kama waziri mkuu wa kipindi cha miezi 20, amefaulu kushinikiza baadhi ya sera muhimu za serikali ya rais Macron, ikiwemo sheria tata ya pensheni, uhamiaji na sheria mpya 30.