Mnamo 8, 2022 Rais wa Ukraine alifanya mahojiano na moja ya chombo cha habari kiitwacho ABC News.
Mtangazaji alisikika akimuuliza “Mheshimiwa Rais asante sana, tunafahamu kinachoendelea nchini Ukraine. Je, hali ikoje leo kwenye uwanja wa vita? Je, unafikiri unaweza kubaki na mji mkuu wa kyiv?”
Rais wa Ukraine aliyayotoa majibu haya..‘Tunapigwa mabomb, sio tu katika jiji la kyiv, sio tu nyumba zetu, lakini pia katika vitongoji. Kwa sasa sababu ya mashambulizi, mji mkuu hautambuliki tena; pia miji ya Kharkhiv, Mariopol, nk‘- Rais wa Ukraine
‘Nina uhakika kwamba waUkraine wako tayari kusimama dhidi ya Warusi kwa maisha yao yote. Katika miji tofauti iliyoshambuliwa, watu wa kawaida hawakuwa na bunduki, lakini walipigana na askari wa Kirusi. Hata askari wa Kirusi hawana ujasiri huo. Tukiwa na askari mmoja wa Ukraine, tunapambana na askari 10 wa Urusi’- Rais wa Ukraine
Ayo TV & Millardayo.com imekuandalia taarifa kamili unaweza ukabonyeza play kufahamu zaidi.
VITA YA UKRAINE NA URUSI, SABABU BIDHAA KUPANDA BEI NCHINI, RAIS SAMIA AFUNGUKA