Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Alhamisi kwamba alitembelea eneo la Kherson ambako maelfu ya watu wanakabiliana na athari za mafuriko kufuatia uharibifu wa bwawa la Kakhovka.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema leo Alhamisi kwamba alitembelea eneo la Kherson ambako maelfu ya watu wanakabiliana na athari za mafuriko kufuatia uharibifu wa bwawa la Kakhovka.
Zelenskyy alisambaza video kwenye mtandao wa Telegraph akikutana na maafisa na kusema walijadili uhamishaji, kurejesha mfumo wa ikolojia wa mkoa na hali ya kijeshi katika eneo hilo.
Hiyo ilifuatia hotuba yake ya Jumatano usiku ambapo alitoa wito wa jibu la Ulimwengu la wazi na la haraka.
Alisema juhudi kubwa zinahitajika ikiwa ni pamoja na usaidizi wa makundi kama vile Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alisema Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg “aliahidi mifumo ya NATO itatumika kutoa msaada wa kibinadamu.” Kuleba na Stoltenberg walitangaza kuwa wataongoza mkutano Alhamisi na washirika wa NATO kujadili hali hiyo.
Gavana wa eneo la Kherson alisema Alhamisi takriban kilomita za mraba 600 zilikuwa chini ya maji.
Gavana Oleksandr Prokudin alisema karibu theluthi mbili ya ardhi iliyofurika ilikuwa kando ya Mto Dnipro unaokaliwa na Urusi, wakati theluthi moja ilikuwa upande ambao bado unadhibitiwa na Ukraine.