Ni Muda huu kutokea Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) ambapo unaendelea Mkutano Mkuu wa Klabu ya Young Africans ambapo Wanachama na Viongozi wamekutana kuzungumza maendelea na mafanikio ya timu yao.
Mkutano huo unaongozwa chini ya Rais wao, Hersi Said.
“Young Africans SC kwa msimu wa 2022-2023 tumeweza kutembelea vituo 20 vya watu wenye uhitaji na kuchangia damu chupa 637 na kuwa Klabu na Taasisi ya kwanza kutambulika rasmi na Wizara ya Afya katika uchangiaji damu kupitia Wanachama, Mashabiki na Wapenzi wa Young Africans SC”- Rais wa Young Africans SC Hersi Ally Said
“Young Africans SC kwa msimu wa 2022-2023 tumeweza kutengeneza kiasi cha Tsh. 3,550,000,000 kupitia mafanikio yatokanayo na ushiriki wa Klabu yetu katika mashindano mbalimbali”- Rais wa Young Africans SC Hersi Ally Said
“Rasmi Young Africans SC imeingia makubaliano na Benki kubwa tatu nchini CRDB, NMB na NBC katika huduma ya Usajili wa Wanachama Kidigitali kote nchini”- Rais wa Young Africans SC Hersi Ally Said