Rais wa zamani wa Burundi Pierre Buyoya amefariki akiwa na umri wa miaka 71, binamu yake na chanzo cha kidiplomasia kimethibitishia taarifa za kifo chake.
Chanzo cha familia kimesema amefariki Mjini Paris, Ufaransa siku ya Alhamisi kutokana na athari za ugonjwa wa Covid-19.
Jenerali huyo mstaafu alihudumu mara mbili madarakani kwa jumla ya miaka 13 baada ya kumpindua mtangulizi wake madarakani
Mwezi October, alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani na Mahakama ya Burundi kwa kosa la mauaji ya rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini humo, Rais Melchior Ndadaye mwaka 1993 -ambayo yalisababisha mauaji ya karibu watu 300,000. Alikana kufanya makosa hayo.