Rais mteule wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameapishwa kwa kipindi cha pili cha miaka mitano madarakani katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi wa kikanda na nchi za nje. Bwana Mnangagwa ameapishwa baada ya kushinda kwa kupata asilimia 52.6 ya kura zote katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita.
Kabla ya hapo mpinzani wake mkuu Nelson Chamisa wa chama kikuu cha upinzani cha CCC aliyepata asilimia 44 ya kura alikataa matokeo ya uchaguzi na kutoa mwito wa kufanya upya uchaguzi, kwa madai ya kuwepo kwa dosari kwenye uchaguzi.
Habari nyingine zinasema, kutokana na mwaliko wa Rais wa Zimbabwe, mjumbe maalumu wa Rais Xi Jinping wa China Bw. Zhou Qiang amehudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais Mnangagwa huko Harare.
Rais Mnangagwa amekutana na Bw. Zhou ambaye amewasilisha pongezi na matumaini mema kutoka Rais Xi.
Inakadiriwa watu elfu 40, walimshangilia Mnangagwa alipowasilil kweye uwanja wa taifa wa michezo mjini Harare. Katika hotuba yake, aliwashukuru wazimbabwe kwa kile alichokiita kuwa uchaguzi wa amani na uwazi. Aliahidi kutumia rasilimali za asili za Zimbabwe ili kuongeza uzaishaji na kuugeuza uchumi wa nchi.