Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Kenya William Ruto ambaye yuko ziarani nchini China kuhudhuria mkutano wa kilele wa baraza la ushirikiano wa kimataifa la “Ukanda Mmoja na Njia Moja”.
Rais Xi amesema urafiki kati ya China na Kenya umekuwa na historia ndefu.
Tangu China na Kenya zianzishe uhusiano wa kibalozi miaka 60 iliyopita, nchi mbili zimekuwa zikiheshimiana na kuungana mikono.
Katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizi zimeshirikiana kutekeleza miradi kadhaa ikiwemo reli ya SGR na bandari ya mafuta ya Mombasa, huku ujenzi wa pamoja wa pendekezo la “Ukanda Mmoja na Njia Moja” umepata mafanikio nchini Kenya na kuwanufaisha watu wa pande mbili.
Amesema China inauangalia uhusiano kati yake na Kenya kwa mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu, na inapenda kushirikiana na Kenya katika kusukuma mbele uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili.
Rais Ruto amepongeza mkutano wa awamu ya tatu wa baraza la ushirikiano wa kimataifa la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na kusema tangu China na Kenya zianzishe uhusiano wa kibalozi miaka 60 iliyopita, pande mbili siku zote zimekuwa zikiaminiana na kuheshimiana.