Rais Volodymyr Zelensky anatarajiwa kufanya mkutano na waziri mkuu Giorgia Meloni na kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis, Hii ikiwa ni ziara ya kwanza kwa kiongozi huyo nchini Italia tangu nchi yake ilipovamiwa na Urusi.
Aidha kiongozi huyo pia amethibitisha kwamba atafanya kikao na rais wa Italia Sergio Mattarella, waziri mkuu Giorgia Meloni na Papa Francis.
Televisheni nchini humo zimeonyesha msafara mrefu wa magari yaliombeba rais Zelensky yakiondoka katika uwanja wa ndege, maofisa wa usalama wakonekana pia kufunga sehemu kubwa ya mji mkuu wa Italia.
Wakati rais Zelensky akiwasili mjini Rome, Ujerumani imetangaza msaada wa silaha zenye kima cha euro bilioni 2.7 kwa ajili ya Kyiv, msaada huo ikijumuisha magari ya kivita na silaha ya za kuzuia mashambulio ya angani.
Licha ya nchi ya Italia, mwanachama wa EU na NATO kuonekana kuwa na uhusiano mzuri na Moscow, nchi hiyo imetuma silaha kwa Ukraine tangu uvamizi wa Urusi mwezi Februari mwaka wa 2022.
Kando na kutuma silaha nchini Ukraine, Italia pia imeonekana kuunga mkono vikwazo vya kiuchumi vilivyotangazwa na mataifa ya Magahribi dhidi ya Urusi.
Waziri mkuu wa Italia, alifanya ziara nchini Ukraine mwezi Februari ambapo alikutana mwenzake wa Kyiv Denys Shmyhal