Huwa matukio kama haya au hisia kama hizi sio rahisi kuonekana waziwazi kwa kiongozi wa nchi pale anapohutubia au kuzungumza na Taifa kwa njia ya TV.
Imetokea kwa rais wa Korea Kusini Park Geun-hye akilihutubia taifa kuhusu kivuko kilichozama April 16 2014 na kuua watu wapatao 300 huku wengi wao wakitajwa kuwa Wanafunzi ambapo kwenye hii hotuba rais aliomba radhi kwa uzembe uliofanyika kwenye vikosi vya uokoaji.
Jumapili iliyopita Rais huyu alihudhuria ibada kanisani kuwaombea waliofariki kwenye ajali lakini pia alikutana na ndugu waliopoteza watoto/ndugu zao kwenye kivuko hicho ambapo waliozembea wanaadhibiwa sheria.
Miili 286 ilipatikana lakini mpaka sasa 18 haijaonekana, watu 172 wakiwemo 22 Wafanyakazi wa kivuko hicho kati ya 29 walinusurika kwenye ajali hii.
Ukitaka kumuona rais mwenyewe akiongea kwa hisia na kutokwa machozi tazama hii video hapa chini
Kama unataka stori kama hizi zisikupite ungana na mimi kwenye twitter kwa kubonyeza HAPA, pia FACEBOOK & INSTA ili niwe nakutumia kila stori inayonifikia.