Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua Mhandisi Ali Said Bakari kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi Zanzibar.
Mhandisi Ali ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe Zanzibar. Uteuzi huo unaanza leo tarehe 18 Mei, 2023.