Klabu ya Simba August 13 wamezungumza na waandishi wa habari katika Press Conference ambayo waliiandaa wao wenyewe, Simba imezungumzia mchezo watakaocheza siku ya Jumamosi ya August 15 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam sambamba na kuweka wazi juu ya hatma ya golikipa Ivo Mapunda na mshambuliaji Elias Maguli ni kweli wametemwa?
“Jumamosi tarehe 15 timu ya Simba inatarajia kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki na timu ya URA ya Uganda mchezo utachezwa Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam saa 10 jioni na timu ya URA inatarajia kuwasili mchana huu kutoka nchini Uganda, maandalizi yote yameshakamilika”>>> Haji Manara
“Kila kitu kipo sawa Simba inatarajia kuutumia mchezo huo kuwajaribu wachezaji wake wawili wapya mshambuliaji mmoja na golikipa”>>> Haji Manara
“Elias Maguli nafikiri kumbukumbu zetu zipo vizuri kabisa Elias Maguli alisajiliwa huu ni msimu wake wa pili ambao utaanza mwezi wa nane kwa mkataba wa miaka miwili ni mchezaji wa Simba mpaka hapa ninapo zungumza ni mchezaji wa Simba kilichotokea ni kwamba wakati tukijiaandaa na mchezo wa Simba Day katika orodha ya mwalimu ya wachezaji 22 aliowataka jina la Elias Maguli halikuwemo”>>>Evans Aveva
“Jina lake halikuwepo kwa vigezo ambavyo mwalimu anavijua na sisi kama wanasimba na stake holder wa mpira siku zote mmekuwa mkipiga kelele viongozi hasa wa vilabu vya Simba na Yanga mmekuwa mkiingilia majukumu ya walimu sisi tukaona tuheshimu hilo pamoja na kwamba Elias Maguli tulimsajili kwa matumaini makubwa”>>>Evans Aveva
“Lakini mwalimu alipokuja akaona uwezo wa Elias Maguli ni mdogo kwa hiyo katika ile mechi ya Villa Elias Maguli hasishiriki kinachofuata baada ya hapo ni maongezi pamoja na viongozi wa Simba kujua hatma yake, Ivo Mapunda ni mchezaji ambae kamaliza mkataba wake alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja” Evans Aveva
“Sisi tuliona ni jambo jema sana kuendelea na Ivo kwa sababu ya uwezo aliouonyesha msimu uliopita hivyo kamati ya usajili ilianza kufanya mazungumzo ya kina ikafikia mahali ambapo ikaonekana Ivo ataendelea kuwa mchezaji wa Simba Sports club katika kipindi kinachokuja”>>>Evans Aveva
“Mazungumzo yalifikia hitimisho na wakakubaliana Ivo atakuja kusaini mkataba na klabu yetu ya Simba mpaka hivi ninavyo zungumza ni kwamba ni bahati usajili umesogezwa mbele kwa hiyo bado tuna muda lakini mpaka hapa ninavyozungumza Ivo bado hajaonekana kuja kusaini mkataba Simba hivyo jukumu hili limerudishwa tena katika kamati husika na maadam usajili umesogezwa mbele na Ivo yupo bado Dar tutatoa majibu”>>>Evans Aveva
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos