Good news kwa mashabikiwa Mbeya City imetangazwa tena leo July 18 2016 kupitia ukurasa wake rasmi wa instagram, Mbeya City ambayo makazi yake ni jijini Mbeya imetangaza kumsajili mchezaji wa Yanga aliyekuwa kwa mkopo katika klabu ya Stand United Rajab Zahir.
Mbeya City imetangaza kumsajili Zahir ikiwa ni wiki kadhaa zimepita toka watangaze kumsajili Mohamed Mkopi kutoka Tanzania Prisons kwa mkataba wa mwaka mmoja. Zahir ambaye ni beki wa kati amejiunga na Mbeya City kwa mkataba wa mwaka mmoja, baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka mitatu na Yanga akiwa kwa mkopo Stand United.
ALL GOALS: YANGA VS MEDEAMA SC JULY 16 2016, FULL TIME 1-1