Rapa wa Uingereza, Michael Ebenezer Kwadjo Omari Owuo Jr., maarufu Stormzy, ameonyesha kuunga mkono Palestina katika vita vinavyoendelea kati ya Israel na Hamas, Islamic Resistance Movement.
Stormzy, ambaye amekuwa nje ya mitandao ya kijamii kwa wiki kadhaa, alirejea Alhamisi usiku ili kuchangia mawazo na kuwapasha mashabiki kuhusu shughuli zake za sasa.
Alisisitiza kwamba wakati wowote kunapokuwa na “ukosefu wa haki” ulimwenguni, sikuzote atakuwa upande wa “walioonewa.”
Kwenye akaunti yake ya Instagram uliothibitishwa, aliandika, “Natumai kila mtu ni mzuri, mawazo ya muda mfupi;
“Palestina Huru;free Palestine
“Katika siku zijazo, ikiwa kutakuwa na ukosefu wa haki waziwazi duniani, hata uwe mkubwa au mdogo kiasi gani, mara 100 kati ya 100, nitakuwa upande wa wanaokandamizwa. Bila shaka. Kama nilivyokuwa siku zote.
Mitandao ya kijamii ni njia nzuri sana ya kutetea kile kilicho sawa, Pia kuna njia nyingine nyingi za kufanya hivyo.
“Nachukia mitandao ya kijamii. Yote hii inaniumiza sana ikiwa mimi ni mwaminifu lakini ninawapenda sana nyie na ni vizuri kuwapo na kuungana nanyi kupitia hiyo.
Stormzy aliahidi kurudi kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni ili kuwapa mashabiki wake update zaidi, “natumai kuwa na muziki mpya.”