Mshambuliaji wa Man United Marcus Rashford ameonesha kuguswa moja kwa moja na janga la mlipuko wa virusi vya corona ambavyo vimekuwa vikihathiri mfumo wa maisha ya kawaida ya wengi duniani.
Rashford ameonesha kuguswa na kuwasiliana na taasisi zinazoweza kufikisha msaada wake kwa watoto wa shule, ametoa uamuzi huo ikiwa kesho UK watazifunga shule zote kwa muda kama njia ya kuepusha msongamano na kuepukana na virusi hivyo.
“Jamani UK nzima kuna zaidi ya shule 32,000 kesho zote hizo zitafungwa, wanafunzi wengi wanaosoma shule hizi huwa wanapewa chakula bure, hivyo nimezitumia siku chache zilizopota kuongea na taasisi namna gani huu uhaba wa chakula utamalizwa” >>> Rashford kupitia twitter