Shirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza rasmi kuwa Taifa la Saudi Arabia litakuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia 2034.
Hata hivyo fainali ya Kombe la Dunia 2030 itaandaliiwa na mataifa matatu Ureno, Hispania na Morocco ambao waliomba kuandaa michuano hiyo kwa pamoja.
“Tunaleta soka katika nchi nyingi zaidi na idadi ya timu haijapunguza ubora. Kwa kweli iliongeza fursa,” Infantino alisema kuhusu Kombe la Dunia la 2030.
Pendekezo la pamoja kutoka Morocco, Uhispania na Ureno litashuhudia tukio la 2030 litafanyika katika mabara matatu na mataifa sita, huku Uruguay, Argentina na Paraguay zikiandaa michezo ya kusherehekea kuadhimisha miaka mia moja ya mashindano hayo.
Saudi Arabia itakuwa taifa la pili Mashariki ya Kati kuandaa michuano hiyo baada ya Qatar kuandaa mwaka 2022.
Toleo la 2034 litafanya mashindano ya kwanza kabisa ya timu 48 katika nchi moja mwenyeji.
Mechi zitafanyika katika viwanja 15 katika miji mitano mwenyeji nchini Saudi Arabia: Riyadh, Jeddah, Al Khobar, Abha, na Neom.