Mshambuliaji wa zamani wa TP Mazembe Mtanzania Thomas Ulimwengu amerudi kucheza soka la Tanzania na kutambulishwa leo Singida kama Mchezaji mpya wa Singida Fountain Gate.
Ulimwengu anarejea kucheza soka Tanzania baada ya miaka 13 kupita akicheza soka nje ya nchi ambapo rekodi zinaonesha amewahi kucheza soka Tanzania kwa kipindi kifupi cha 2009-2010.
Baada ya hapo Ulimwengu alijiunga na vilabu vya TP Mazembe (2011-2016), AFC Eskilstuna ya Sweden (2017), Sloboda Tuzla ya Bosnia (2017-2018), Al Hilal ya Sudan (2018), JS Saoura ya Algeria (2019) na TP Mazembe tena (2020-2022).