Inasemekana kwamba Rasmus Højlund anataka kujiunga na Manchester United, na ni jambo la wazi tangu siku ya kwanza ya mazungumzo na siku hizi za mwisho za juma zinaweza kuwa muhimu.
Zabuni ya PSG haijabadilisha mawazo ya Højlund kwa hatua hii kwani sasa Manchester United iko tayari kwa duru mpya ya mazungumzo na Atalanta kufuatia ombi lao la awali la euro milioni 60.
Hata hivyo, Mashetani Wekundu watakuwa na ushindani kutoka kwa wababe wa Ufaransa PSG kuwania saini ya Mdenmark huyo.
Wakati huo huo, United wanakaribia kumsajili kiungo wa Fiorentina Sofyan Amrabat, kulingana na ripoti.
Kwingineko, mazungumzo ya kuchukua madaraka yanaendelea kusuasua, huku Glazers bado hawajatoa tangazo lolote baada ya kupokea zabuni zilizoboreshwa.