Mkuu wa Mkoa wa DSM Albert Chalamila akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamepokea msaada wenye thamani ya Milioni 35 kutoka kwa süperstar Zari The Boss Lady akiwa kama Balozi wa kampuni ya Softcare iliyeshirikiana naye kufanya hivyo msaada ambao umeambata na ofa ya kuwasaidia watoto wote watakao zaliwa katika hospitali hiyo kupata Diapers bure kwa kipindi cha Mwaka mmoja…
Zari ambaye amefunguka kwa kusema yeye kama mama amekuwa akiguswa sana kuona baadhi ya wazazi wakijifungua na kutokana na ugumu wa Maisha wamekuwa wakikosa baadhi ya huduma Muhimu kWa watoto wao hivyo kuiomba kampuni ambayo amekuwa akifanya nayo kazi kwa muda mrefu kuweza kusaidia wakinamama zaidi
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa DSM Albert Chalamila ambaye amepokea msaada huo amesema kitendo cha yeye kukubali kuwa mgeni Rasmi Kwenye shughuli hiyo ni Ishara tosha kuwa atakua atatumika kama Balozi wa kampuni hiyo hivyo huwa hapokeagi misaada midogo midogo na Kwenye hili ambalo Zari na kampuni anayoifanyia kazi wamefanya amewaomba kuongeza nguvu tena kwa upande ma tatizo mengine yanayowakuta watoto
Kwa upande wa Prof Janabi ameshukuru sana kwa msaada huo kwani ungeweza kuwasaidia wakina mama huku akiomba kitengo cha kuwahudumia watoto pale Muhimbili basi na chenyewe kipewe hadhi ya kuwa hospital ya watoto ya kitaifa kutokana huduma zake kukidhi vigezo