Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rc Ayoub Mahamoud amelazimika kurudi mkoa aliohamishwa Baada ya Teuzi ya Rais ambapo alipokua akihudumu nafasi ya uku wa mkoa wa Kaskazini Unguja kufuatia ahadi aliyoitoa wakati akihudumu kama Mkuu wa Mkoa wakati wa ziara ya Spika wa Bunge la Tanzania Dkt Tulia Ackson baada ya kuahidi mifuko 800 ya saruji
Ayoub licha ya kua Mkuu wa Mkoa mwingine wa kusini amelazimika kutoa mifuko 800 ya saruji kwa ajili ya jengo la chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini A katika eneo la Chaani huku akibainisha sababu za kurudi mkoani humo ni kuona jengo hilo bado linachelewa kwishaa na kwamba saruji hizo zitaweza kukamilisha jengo hilo ambalo litakua na ghorofa
kwa upande wake Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Kaskazini Iddi Ali Ame amesema saruji hiyo itakamilisha jengo hilo na kwa yeyote atakae bainika kuitumia saruji hiyo kinyume na lengo atakua amejiumiza kwa kushughulikiwa kwa utaratibu wa chama.