MTU mmoja amefariki papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne ikiwemo lori la mafuta na hiace pamoja na bajaji mbili, barabara kuu ya Tanzam eneo la Mbembela katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa nne asubuhi ambapo lori lililobeba mafuta lilifeli breki na kuyaparamia magari yaliyokuwa mbele yake ikiwemo haice ambayo ilisababisha kifo cha dereva papo hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema Serikali imetenga kiasi cha fedha Shilingi Bilioni 7.5 ili kukabiliana na tatizo la ajali ambapo kwa awamu ya kwanza itajengwa barabara yenye urefu wa Kilomita 16.5 na awamu ya pili itajengwa ya Kilomita 40.