Mkuu wa mkoa wa kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahamoud amefikia uwaamuzi wa kuwapatia wafanyakazi wa ofisi hiyo chai ya asubuhi (vitafunwa vya mikate ,siagi na chai utaratibu ambao amesema rasmini utaanzia kesho jumatatu may 6 ,ili kupunguza kudhurura na kuongea na simu maara kwa maara pamoja na kutoka nje kwenda kununua urojo
Rc Ayoubu ameyasema hayo wakati akifungua kampeni ya watumishi wa serikali ya amsha amsha kusini ambayo yenye lengo la kutokomeza uchelewaji makazini kuzurura matumizi ya simu vitu ambavyo amesema haridhishwi navyo kwa watumishi na kuahidi kuanza kugawa chai asubuhi fedha ambazo zitatoka kwenye mshahara wake
” nitaanza jumatatu ya tarehe 6 na sitatoa kwenye mfuko wa serikali nitatoa kwenye sehemu yangu ya mshahara wangu kuweza ili kuleta ufanisi kwenye ofisi uwajibikaji watumishi wengi baada ya kupata mshahara siku chache wanakua hawana pesa ndio maana wanapata shida ya kuhangaika ya huku na kule –Rc Kusini Unguja Ayoub Mohammed “