Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu Wakurugenzi na waweka hazina wanaodaiwa kukusanya mapato ya Halmashauri na kuyafanyia matumizi bila kupitia benki kwani ni kinyume na maelekezo ya Serikali.
Akizindua kikao cha baraza la Madiwani Wilaya ya Uyui Dkt. Sengati amepiga marufuku ya matumizi ya fedha zilizokusanya na Halmashauri bila kupitia benki.
“Baadhi ya Wakurugenzi au waweka hazina wanaruhusu utaratibu wa kukusanya mapato na kuyagawia kamisheni kutoka katika makusanyo yaliyokusanywa kabla hayajapitia benki hili halikubaliki” Dkt. Sengati RC Tabora