Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego ametembelea vituo vya mageti ya ukusanyaji mapato katika halmashauri ya Wilaya ya Iringa na Wilaya ya kilolo kujionea kazi ya ukusanyaji mapato zinazofanyika na amewataka wanannchi wasiwe wakwepaji kodi
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo wakati alipokuwa akikagua na kupata taarifa za vituo vya ukaguzi katika halmashauri ya wilaya ya Iringa na ametoa onyo kwa wananchi wanao kwepa kodi za serikali kwa maksudi kuwa watashughulikiwa ipasavyo na awako tayari kuona serikali inapoteza mapato ya taifa kwa uzembe wa watu wachache kwa maslahi Yao binafsi.
“ Sisi kama mkoa wa Iringa tumejipanga vyema kwasababu tunajukumu kubwa katika ukusanyaji wamapato na ole wa mtu anayekwepa ulipaji kodi kwa namna moja au nyingine sheria zipo na ikibainika sheria zitafuatwa na adhabu zitatolewa kwa watu wakwepaji wa kodi ivyo basi wafanya biashara waaache visingizio kwenye utoaji kodi “ Rc Dendego
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego amewapongeza viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Iringa ikiongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Wakili Bashir Mhoja na viongozi wa Tra kwa kazi kubwa wanayoifanya ya ukusanyaji wa mapato ya serikali