Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira amethibitisha kupata maambukizi ya virusi vya Corona baada ya kufanya vipimo hivyo hivi karibuni.
“Nimepima na matokeo yamekuja yameonesha nimeambukizwa virusi vya corona, sioni dalili za ugonjwa sina homa sikohoi lakini vipimo vimeonesha, hii ni dalili kwamba Watu wengi tunaweza kuwa tunetembea tukiamini tuko salama kumbe hatuko salama, sijui niliambukizwa lini “ – RC Mghwira