Mkuu wa Mkoa wa Tanga waziri kindamba amezindua mikopo ya garama nafuu kwa wafanyabiashara wadogo wa soko la Tangamano na kuwataka wafanyabiashara hao kutumia mikopo hiyo kwenye malengo yalio kusudiwa ili iweze kuwa na tajia kwenye biashara zao.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mikopo hiyo inayo tolewa na bank ya CRDB kwa wafanyabiashara wadogo katika viwanja vya tangamano mkuu wa Mkoa Waziri kindamba alisema kuwa kuwepo mikopo ya gharama nafuu kwa wafanyabiashara wadogo itawawezesha kukua kiuchumi na kurudisha marejesho kwa wakati.
“kwa wale watakao bahatika kupata mikopo hii naomba mkaitumie kwa madhumuni yaliokusudiwa ili muweze kufanya marejesho kwa wakati na kuendelea kutunza uamini mliopewa na niseme tu ukweli wanawake ni walipaji wazuri wa marejesho kuliko wanaume hivyo naomba wanaume wenzangu mkipata mikopo rudini nyumbani mkae na wake zenu ili muweze kupanga njia bora ya matumizi na namna bora ya kurejesha”Alisema kindamba.
kwaupande wake meneja wa kanda ya kaskazini wa CRDB cosimasi Sadati amesema kuwa lengo la mikopo hiyo ni kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kuondokana na mikopo ya kausha damu ambayo ina watesa huko mitaani ambapo sambamba na hilo wametoa reflector 250 kwa bodaboda wa jiji la Tanga ili kuweza kutambulika kwenye vituo vyao na kuweka usalama kwa watumiaji.