Mhe. Abubakar Kunenge Mkuu wa Mkoa wa Pwani leo Mei, 2 2023 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua Mazingira ya Kituo cha Mabasi kibaha (Kibaha Bus Terminal).
Akiwa kwenye ukaguzi huo Kunenge amesikiliza kero za Wananchi waliokuwemo eneo hilo. Kero hizo ni pamoja na Kuchelewa kufika kwa Mabasi ya Mwendekas kituoni hapo ambayo yanafanya safari zake Kati Kibaha DSM. Wananchi hao wemeeleza kutotosheleza kwa vikingia jua na Mvua zilizojengwa kwenye Eneo hilo na Kujaa kwa maji kwa baadhi ya maeneo yanayotumiwa na Mabasi ya mwendokasi na Mabasi madogo kwenye eneo hilo.
Akijibu kero za Wananchi Kunenge ameeleza Nia ya Mhe Rais na wasaidizi wake ni kutatua kero za Wananchi na kuwarahisishia utoaji wa Huduma. Ameeleza kero zote amezichukua na zinakwenda kufanyiwa kazi. Kuhusiana na Mabasi ya Mwendokasi amewasiliana na mamlka husika kwamba Huduma hiyo kwa sasa hairidhishi na hivyo wameahidi kuongeza Mabasi hayo na Viongozi wa DART kutembelea eneo hilo. Kuhusu kuharibika kujaa maji na mabonde kwenye Kituo hicho ameagiza wataalma wa Halmshauri kushirikiana na TANROADS na TARURA kufanya matengenezo ya maeneo yaliyoharibika. Amemtaka Mkurugenzi wa Mji kuangalia upya vikingia mvua na jua na kufanya maboresho.