Mhe. Abubakar Kunenge Mkuu wa Mkoa wa Pwani leo Agosti 7,2021 ameshiriki kwenye Mazishi ya Watoto watano waliofikwa na mauti kwenye Ajali iliyohusisha Pikipiki na Fuso Eneo la Kata ya Kimange Halmashauri ya Chalinze.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa Ameeleza kuwa Mnamo Tarehe 6 Agosti, 2021 majira ya saa 1 :15 Jioni Gari aina Mitusubish Fuso Na 198 CWN ikitokea Dar es salaam kwenda Arusha iligonga Mwendesha Pikipiki kusababisha vifo vya Wanafunzi wanne pale pale na mmoja kufariki akipatiwa matibabu Hospital ya Jeshi Kihangaiko.
Ameeleza kuwa Wanafunzi hao watano wa Kimange Sekondari walikuwa wamepakiana kwenye Pikipiki wakitokea Kimange kuelekea Mbwewe. Wanafunzi hao walikuwa wakitokea michezoni shule Jirani ya kwamakocho Sekondari.
Wanafunzi hao waliofariki ni Laya Ubwa Masudi (16) mwanafunzi wa kimange Sekondari Kidato cha tatu, Furaha Athumani (16) Mwanafunzi Kimange Sekondari Kidato cha tatu, Athumani Bushiri (15) Mwanafunzi kimange Sekondari Kidato cha Kwanza, Amina Msomba (15) Mwanafunzi Kimange Sekondari Kidato cha Kwanza na Athumani Mchafu (17) Mwanafunzi Kidato cha tatu.
Ameeleza kuwa Chanzo cha Ajali hiyo ni Uzembe wa Dereva wa Gari na mwendo kasi uliosababisha kushindwa kumudu Gari hilo na kupelekea kumgonga Mwendesha Pikipiki akiyekuwa mbele yake.
Amethibitisha kuwa Jeshi la polisi limefanikiwa kumshikilia Dereva wa Gari hilo kwa ajili ya hatua za kisheria.
Kunenge ametoa pole sana kwa Familia na Wananchi wa Kata hiyo kwa Msiba Mkubwa ambao wameupata.
“Kwa niaba ya Mhe Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan nitoe pole nyingi kwenu, kubwa zaidi kwetu ilikuwa ni kuja kushiriki nanyi, tumekuja na Swadaka Ndogo kwa ajili ya kufariji Familia hizi.
“Yaliyotokea yametokea, niwaombe tuzingatia matumizi ya vyombo vya Moto. Sisi kwa upande wa Serikali tunaendelea kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria za Nchi. Dereva wa Gari hilo tunaye tutachukua hatua” Alisema Kunenge.
CHAMA AMKWAZA MO DEWJI, AMJIA JUU “MANARA NDIO ANAKULIPA?”