Mkuu wa Mkoa wa Arusha paul Makonda amechukizwa na utendaji kazi wa watumishi wa serikali wa Mkoa wa Arusha nakusema atakutana nao kwenye kikao cha ndani
Makonda ameshindwa kuwaelewa baadhi ya watumishi walivyokuwa wanajieleza nakutoa taarifa za miradi Wakati akizungumza na watendaji wa mamlaka mbalimbali za serikali za mitaa na watendaji wa taasisi mbalimbali za umma Mkoani Arusha kwa lengo lakufanya tathimini
Hata hivyo amemueleza Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Missaile Musa hajakubaliana na utendaji kazi wa watumishi wa Mkoa wa Arusha nakusema endapo angekuwa na uwezo, angewafukuza kazi zaidi ya nusu ya wafanyajazi wa idara ya ardhi nakuiendesha kama kampuni ili kurudisha uwajibikaji
“Ndugu leo hapa nikitaka kujua maeneo ya uwekezaji naweza kupata majibu zaidi ya matatu katika taasisi moja inayofanya kazi moja ndani ya serikali hii hapana tunachelewa kuwaletea wananchi maendeleo kwa sababu watumishi hawawajibiki pamoja “
Kutokana na hali hiyo Makonda amelazimika kuahirisha Mkutano wake wa kuendelea kusikiliza wakuu wa taasisi mbalimbali zilizopo na kuahidi kukaa na watendaji wa mkoa huo ili kujengeana uwezo wa namna ya kuzungumza na kuwasilisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa maelekezo na mipango ya serikali.