Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima amewataka wanawake wa Kiislam Mkoa wa Morogoro kuwa na mfano bora katika Jamii kwa kutenda matendo mema pamoja na malezi bora kwa watoto.
Rc Malima ameyasema hayo wakati akihutubia Baraza la Wanawake wa Waislam Mkoa Morogoro lililofanyika katika Msikiti mkuu wa ijumaa Bomaroad uliopo.mjini Morogoro.
Malima amesema vitendo vinavyofanywa na baadhi ya Vijana wakiume havina maadili ambapo amewataka wazazi kutenga muda wa kuzungumza na Vijana hao Ili kubadili mfumo wa tabia
Aidha Rc Malima amewataka akinamama hao kuwa na umoja na ushirikiano baina yao kwa sababu wao ni nguzo muhimu katika Jamii katika kufanikisha vita ya kutokomeza vitendo hivyo vichafu katika jamii ya watanzania.
Kwa Upande wake mkuu wa Wilaya Morogoro Rebeca Nsemwa amewataka akina mama hao kuunda vikundi Ili waweze kunufaika na fedha za mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri
Naye Katibu wa Baraza la Wanawake la Wailsam Manispaa ya Morogoro Bi. Amina Hussein amesema baraza Hilo limekua likikutana Kila mwaka mara Moja lengo kuwakutanisha wanawake wa kiilsam Kujadili masuala mbalimbali ikiwemo suala la malezi Kwa Vijana