Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amepiga marufuku wanafunzi kurudishwa nyumbani na kushindwa kuendelea na masomo kwasababu za mzazi kushindwa Kuchangia Chakula shuleni.
RC Sendiga ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Galapo ambapo amesema suala la watoto kula shuleni haliwezi kuepukika “Maelekezo ya Serikali nimarufuku mzazi kukwepa jukumu la mtoto kula shuleni lakini ni muhimu Wazazi na Kamati za shule zikae pamoja kujadili namna bora ya kuwahudumia wanafanzi chakula shuleni kulingana na hali ilivyo na sio waalimu kupanga utaratibu wanaoutaka wao,sitaki kusikia mtoto anafukuzwa shuleni waiteni wazazi mtengeneze Kamati maalumu kwaajili ya kuratibu namna ya upatikanaji wa chakula shuleni”
Hatua hiyo imekuja baada ya Wananchi kulalamika wanafunzi kurudishwa nyumbani kwa kushindwa Kuchangia chakula shuleni.
“Watoto wapo mtaani wamefukuzwa shuleni Wazazi hawana chakula,Mzazi anaenda kununua Kilo moja akale yeye na watoto na apeleke shuleni atapata wapi? hatuna kazi wala vibarua na mavuno shambani hakuna kumekauka,tunaomba hili ulifanyie kazi Mama”