CHAMA cha Walimu nchini (CWT), kimeunga mkono maono ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ya kuanzisha Shule maalumu za Sekondari katika kila Halmashauri ya Mkoa huo ambazo zitakuwa zinapokea Wanafunzi wanaofanya vibaya kwenye Mitihani ya Kidato cha nne.
Hivi karibuni Chalamila aliagiza Maofisa Elimu Sekondari na Msingi wa Halmashauri zote za Mkoa huo, kuandaa mipango ya ujenzi wa shule hizo ambazo zitakuwa zinapokea Wanafunzi wanaopata daraja sifuri na daraja la nne kwenye mitihani ya kidato cha nne.
Amesema wanafunzi hao watakaokuwa wanapokelewa kwenye Shule hizo watakuwa wanasoma miaka miwili yaani kidato cha tatu na nne kisha wanarudia kufanya mtihani wa Taifa na wakifaulu wanaendelea na masomo.