Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amesema bado nia yake ya kukutana na watengenezaji wa pombe aina ya gongo iko palepale, lengo likiwa ni kujadiliana nao na kuona namna nzuri ya kuiboresha pombe hiyo kwa kuwapelekea TBS na Mkemia na kuipima, kuondoa sumu na kisha kuibrand.
“Kwanini gongo haitambuliwi kama kinywaji halisi cha Kitanzania!, badala ya kukuza na kuona kuwa hapa kuna kitu kinaweza kutupeleka kwenye viwanda tunazuia, mnaokunywa hizo pombe za viwandani mnajua origin yake?,nitakutana na watengeneza gongo tuone namna ya kuiboresha”-RC Mtwara
“Nasisitiza nitakutana na watengenezaji wa gongo, kama unamfahamu mwambie aje tuzungumze jinsi ya kuiboresha zaidi na ituletee faida, hatuwezi kuwa na Tanzania ya viwanda ya zuiazuia, tunapaswa kuwa na Tanzania ya Viwanda ya wezeshawezesha“–RC Mtwara
EXCLUSIVE: WAZAZI WANGU WAMENITENGA KISA WANANGU WALEMAVU, BABA ANATAKA KUNIFUNGA, NIMELETA NUKSI