Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Peter J. Serukamba leo tarehe 10/01/2023 amezindua miradi miwili ya maji ya kata za mtunduru na irisya jimbo la singida magharibi yenye thamani ya zaidi ya Milioni 740 katika hafla iliyofanyika katika maeneo yenye miradi
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa miradi hiyo Mhe. Serukamba amemshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa bilioni mbili kwa wilaya ya ikungi kugharamia miradi ya maji na kuwataka wananchi kutunza miundombinu ya maji ili iweze kudumu kwa muda mrefu
Aawali akimkaribisha mkuu wa mkoa kuzindua miradi hiyo, mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro amesema fedha zote za miradi zilizoletwa zimesimamiwa ipasavyo na kazi imefanyika na miradi yote imekamilika kulingana na thamani halisi ya fedha
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri wilaya ya Ikungi mheshimiwa ali juma mwanga amesema kukamilika kwa mradi huo kutawasaidia wananchi wake wa kata ya irisya kupata maji safi na salama kwa ukaribu zaidi