Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela ameruhusu uganga na masuala ya kidini kufanyika katika mashindano ya SHIMMUTA kama kuna timu kutoka Shirika lolote inadhani inaweza kupata ushindi kwa njia hiyo.
Akizungumza mbele ya Viongozi wa timu za mshirika ya umma nchini yanayounda umoja wa SHIMMUTA ambao wamewasili mkoani Tanga kwa ajili ya kuanza mashindano hayo yatayotimua vumbi kwa muda wa siku 14 kuanzia leo 16 hadi 28 mwezi huu wa Novemba na kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ijumaa ya Tarehe 20.
Shigela amesema kila timu ionyeshe uwezo wake ili ipate ushindi wa halali na ni marufuku kwa mchezaji au wachezaji kutumia dawa za kusisimua misuli na atakaye bainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua na vyombo vya dola lakini atakaye tumia njia za asili kama Waganga wa jadi huyo ataruhusiwa kwa Mkoa wa Tanga ni wataalamu wa maswala hayo.