Ni july 26,2016 ambapo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikutana na waandishi wa habari kuzungumzia kuhusu barua ya agizo la waziri wa nchi TAMISEMI juu ya kusimamia uendeshaji wa mradi wa machinga Complex.
Akiongea mbele ya waandishi wa habari alisema…’Nimebaini kwamba majengo ya sasa ya machinga complex hayakujengwa kwa ukubwa sawa na ule ambao halmashauri ya Jiji na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) walikubaliana kwenye mkataba na kupitia kifungu cha 1.1 cha barua ya makabidhiano kinachoeleza kwamba jengo lililokabidhiwa lina sehemu yenye ghorofa 5′– RC Paul Makonda
‘Ghorofa 6 ili liweze kumudu idadi ya machinga wasiopungua 10,000 wakati hali halisi baada ya kutembea jengo hilo ni kwamba jengo lina ghorofa 4 zinazobeba machinga 4,000’>> RC Paul Makonda
‘Kuhusu gharama za mradi nimebaini kuwa fedha za mkopo ziliongezeka toka shilingi bilioni 12.14 za kwenye mkataba na kufikia bilioni 12.7 ikiwa ni nyongeza ya shilingi milioni 560, nyongeza ambayo ilifanyika bila makubaliano yoyote kati ya mkopeshaji na mkopaji’– RC Paul Makonda
ULIIKOSA HII YA RC PAUL MAKONDA KUHUSU WAMACHINGA BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA