Wakala wa nishati vijijini REA imeshatumia Zaidi ya bilioni 70 kwaajili ya kufikisha umeme vijiji vya mkoa wa Manyara kupitia mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu mzunguruko wa pili huku Zaidi ya vijiji 410 kati ya vijijini 440 vimefikiwa na umeme mkoani Manyara
Akiongea katika hafla ya kuwasha vijiji saba kwa mara ya kwanza ndani ya jimbo la mbulu vijijini mkoani manyara mkurugenzi mkuu wa wakala wa nishati vijijini REA mhandisi Hassan Saidy amesema mpaka ifikapo mwezi sita mwaka huu watakua wamewasha umeme vijini vyote 440 vya mkoa wa manyara na kuwataka wananchi kutumia umeme huo kama fulsa ya kiuchumi.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Mbulu vijijini Flatei Massay amesema umeme utaweza kuwaongezea thamani ya mazao yao kutoka kutokana na jimbo hilo kutegemea kilimo,ufugaji na ufugaji wa nyuki kwa wananchi wake.