Real Madrid hawana nia ya kumruhusu Vinícius Júnior kuondoka katika klabu hiyo — hata kama watapewa ada ya uhamisho ambayo itavunja rekodi ya dunia, ripoti ya Diario AS.
Vinícius amekuwa shabaha ya hivi punde zaidi kwa vilabu vya Saudi Pro League, na mchezaji wa Real Madrid yuko tayari kuzingatia pendekezo la kuhamia huko, Al Ahli wanajaribu kumshawishi mshambuliaji kuchukua hatua hiyo kwamujibu wa ESPN.
Uhamisho huo wa rekodi ya dunia unashikiliwa na Paris Saint-Germain, ambao walianzisha kifungu cha Neymar cha euro milioni 222 kumsajili Mbrazil huyo kutoka Barcelona mnamo 2017.
Hata hivyo, tangu hatua hiyo ya mshtuko vilabu vimeweka viwango vya juu vya uhamisho ndani ya mikataba. Real Madrid wanakataa kufanya makubaliano, wakiiambia Al Ahli kwamba kifungu cha kutolewa kwa Vinícius ni pauni bilioni 1.
Vinícius alifunga mabao 24 katika mashindano yote akiwa na Madrid mnamo 2023-24 na amekuwa mchezaji muhimu wa klabu hiyo tangu ajiunge nayo mwaka 2018, akifunga katika fainali mbili za Ligi ya Mabingwa.