Klabu ya Real Madrid imeendelea kuwa klabu tajiri zaidi duniani kwa msimu wa tisa mfululizo, kwa mujibu wa orodha ya vilabu tajiri iliyochapishwa na kampuni ya uhasibu ya Deloitte.
Klabu nyingine ya Uhispania, Barcelona inashilikia nafasi ya pili ikifuatwa na Bayern Munich ya Ujerumani katika nafasi ya pili na tatu.
Kwa mara ya kwanza mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Manchester United ambayo kwa sasa imekabiliwa na msururu wa matokeo mabaya katika ligi kuu ya ngland, imeshushwa hadi nafasi ya nne miongoni mwa vilabu tatu tajiri zaidi duniani kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka kumi na saba iliyopita.
Waandishi wa habari wanasema kuwa ligi ya vilabu vingi kuzalisha kiasi kikubwa cha fedha, nyingi ya vilabu hivyo vinaendelea kupata hasara kubwa kutokana na gharama za mishahara na malipo ya usajili wa wachezaji.