Real Madrid “wanatuma maskauti wao mara kwa mara” kumfuatilia mlinzi wa Lille Leny Yoro, mtaalam wa uhamisho Fabrizio
Romano alichapisha Alhamisi, akimtaja kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 kuwa mmoja wa “walengwa wakuu” wa klabu hiyo ya LaLiga.
Madrid wamekuwa wakihusishwa na Yoro mara kwa mara msimu huu, wakilinganishwa na Raphael Varane, ambaye alihamia Santiago Bernabeu kutoka klabu nyingine ya Ufaransa, Lens, akiwa na umri sawa mwaka 2011.
Hata hivyo, Romano alisema kuwa Madrid itakabiliana na ushindani wa kuwania saini ya Yoro kutoka Paris Saint-Germain, ambao wamekuwa wakifanya kazi ya kumnunua mchezaji huyo tangu Januari.