Franco Mastantuono ana “sifa zinazofanana” na Angel Di Maria na Lamine Yamal, mkurugenzi wa akademi ya River Plate ameiambia Diario AS. huku kiungo huyo akihusishwa kuwindwa na Real Madrid.
Mastantuono, 16, tayari ameingia kwenye kikosi cha kwanza cha River na kumekuwa na ripoti katika wiki za hivi karibuni kwamba anaweza kuhamia Bernabéu hivi karibuni.
Hermes Desio alisema kijana huyo wa kimataifa wa Argentina “ana kila kitu cha kufanikiwa” katika kiwango cha juu zaidi.
“Anaweza kuwa kama Angel Di Maria, mchezaji mzuri na mwenye kipaji cha mguu wa kushoto,” Desio alisema. “Anapenda kukata ndani kutoka winga ya kulia… Akichezea kikosi cha kwanza cha River akiwa na umri wa miaka 16 inaonyesha ana kitu maalum.
“Ana sifa zinazofanana na Yamal, pamoja na kucheza chenga na ubunifu wake… Ni dhahiri kwamba ana furaha hapa na anakua sana, lakini wachezaji wa Argentina wamezoea kuondoka mapema. Kwa kawaida siingii katika hilo.”