Ligi Kuu Hispania imeendelea leo January 31 kwa michezo kadhaa kuchezwa nchini Hispania, klabu ya Real Madrid ya Hispania ilikuwa katika dimba lake la Santiago Bernabeu kuwakabili Espanyol, Real Madrid ambao wapo nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Hispania waliingia dimbani kuhakisha hawapotezi wala kuacha point hata moja ili waweze kuwa na nafasi nzuri ya kuwaombea FC Barcelona na Atletico Madrid wafanye vibaya.
Real Madrid wakiwa chini ya kocha wao Zidane wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 6-0 dhidi ya Espanyol na kutimiza jumla ya point 47 huku wakiwa nafasi ya tatu kwa tofauti ya pont nne na wapinzani wao FC Barcelona wanaoongoza Ligi lakini wapo nyuma mchezo mmoja.
Kikosi cha Zidane ambacho safu yake ya ushambuliaji iliongozwa na Cristiano Ronaldo ambaye kafunga hat-trick, walianza kupata goli la kwanza dakika ya 7 kupitia kwa Karim Benzema, baadae Cristiano Ronaldo aliyefunga goli la pili dakika ya 12 na baadae akafunga magoli mengine mawili dakika ya 45 na 82, baada ya James Rodriguez kufunga goli la tatu dakika ya 16, goli la sita Espanyol walijifunga wenyewe dakika ya 87 kupitia kwa Oscar Duarte.
Video ya magoli ya Real Madrid Vs Espanyol
https://youtu.be/z9butUEGcs8
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.