Mwanaharakati wa Tanzania wa kupinga ndoa za utotoni, Rebeca Gyumi ambaye ni Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali, Msichana Initiative linalotetea haki za wasichana kupata elimu ameshinda tuzo ya umoja wa Mataifa inayotolewa kupitia UNICEF katika kipengele cha mabadiliko ya kijamii.
Mwanzoni mwa mwaka 2016 Rebeca Gyumi kupitia kwa wakili Jebra Kambole wa Law Guards Advocates, walipinga kifungu cha 13 na 17 vya sheria ya ndoa kinachoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa kibali cha mahakama, na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi.
July 08 2016 Mahakama Kuu ilitoa hukumu ikikubali kwamba vifungu hivi vya sheria ya ndoa vinapingana na katiba ya nchi kwa kuweka umri tofauti wa kuoa/kuolewa kati ya mtoto wa kike na wa kiume. Mahakama pia iliitaka serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu kujipanga ili kuvirekebisha vipengele hivi tata ndani ya mwaka mmoja.
ULIKOSA HII YA REBECCA GYUMI BAADA YA KUSHINDA KESI YA KUPINGA NDOA ZA UTOTONI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI