Kwenye magazeti ya leo stori nyingine kubwa ambayo imepewa headline pia kwenye Gazeti Mwananchi ni stori kutoka Mbeya ambayo inahusu aina ya mavazi yaliyopigwa marufuku na hospitali ya Rufaa ambayo iko kwenye Mkoa huo.
Hospitali ya Rufaa Mbeya imechapisha mabango kwenye milango mikubwa ya kuingia kwenye hospitali hiyo ambayo yameandikwa hivi>>’Ni marufuku kwa mwanaume yoyote kuingia hospitalini hapa akiwa amevaa suruali ya mlegezo,kaptula fupi maarufu kama vipensi na wale waliosuka nywele pia wanaovaa bangili nyingi mkononi na heleni’
Bango linalowahusu wanawake limeandikwa hivi>>’Wanawake wote watakaokuwa wamevaa suruali za kubana, sketi fupi maarufu kama vimini na nguo zenye mipasuo mikubwa inayoacha wazi mabega na vifua wazi pamoja na blauzi zinazoacha vitovu nje hawataruhusiwa kuingia Hospitali hapa kupatiwa huduma yoyote’
Ofisa uhusiano wa hospitali hiyo Alinanuswe Mwansasu amesema maelekezo hayo yanawalenga zaidi wafanyakazi wa hospitali hiyo na ndugu wa wagonjwa waliolazwa na wanaowaleta kupata matibabu.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.